Jumapili, 7 Januari 2018

KILIMO CHA MKONGE TANZANIA

KILIMO CHA MKONGE
MUWASILISHAJI; MBARAKA BATARE
KUTOKA; KITUO CHA UTAFITI WA KILIMO MLINGANO
IDARA YA MKONGE
SLP 5088 TANGA TANZANIA
PHONE; 0717698998/0769323117
UTANGULIZI KWA UJUMLA KUHUSU ARI MLINGANO
Kituo cha Utafiti Mlingano ni kituo cha serikali kikonge kilichoanziswa mwaka 1934 kikiwa na idara moja ya mkonge mpaka sasa kinajiusisha na utafiti katika idara kuu tatu utafiti wa mkonge, rutuba ya udongo (soil fertility) na asilimali ardhi (land survey) ili kuiweza jamii ya watanzania Kulima kwa tija na kupata mazao bora na mengi ili kuendeleza vipato vyao kwa mmoja mmoja na kwa taifa pia



KILIMO CHA MKONGE TANZANIA
UTANGULIZI WA ZAO LA MKONGE
Zao la mkonge liliingizwa nchini mwaka 1892 na mtaalamu wa kijerumani Dr. Richard Hindorff ambaye alikuwa ni mtafiti wa mimea na udongo. Mtaalamu huyo alichukua miche 1000 kutoka pwani ya Mexico kwenye jimbo la Yuctan ambalo ambalo ndilo asili ya jina katani na kuisafisha kwa magendo kwa kupitia Frolida , Marekani na Humburg Ujerumani. Kati ya miche 1000, ni miche 62 tu ndiyo iliyofika Tanganyika na ilipandwa sehemu iitwayo kikokwe huko Pangani Tanga. Mkonge ulisambaa maeneo mengi ya Tanganyika mpaka kufikia mwanzoni mwa  miaka 1960 Tanganyika ilikuwa inaongoza kwa uzalishaji wa mkonge ikifatiwa na Brazil na mexico kwa mauzo ya tani 230,000 kwa mwaka nje ya nchi . Kutokana na sababu mbalimbali zilizo jitokeza miaka ya 1970 uzalishaji ulipungua toka tani 230,000 hadi tani 19,700 kwa mwaka 1997. Hata ivyo mageuzi ya kiuchumi yaliyoanza miaka 1980 ambayo yalilenga katika ubinafisishaji na biashara huria , uhuru wa taasisi za kifedha za ndani na nje ya nchi yalifufua kilimo cha mkonge na hasa kukamilika kwa ubinafishaji mwaka 2005 uzalishaji umepanda hadi kufikia tani 40,000 mwaka 2015 hii inatokana na kuongezeka kwa mahitaji ya mkonge na bidhaa zake pamoja na kupanda bei kwenye soko la dunia pamoja na ndani. Soko kuu la mkonge wa Tanzania ni china, Saudi Arabia , India, Uhispania, Ujerumani, Uingereza, Kenya, Uganda na Nigeria.
KWANINI ZAO LA MKONGE
Kutokana na mabadiliko makubwa ya hali ya hewa kwa sasa wakulima wengi wamekuwa wakikosa mavuno kutokana na kutegemea mvua ambazo kwa sasa mtiririko wake siyo mzuri ivyo wataafiti wa mkonge tunahamasisha kilimo cha kilimo cha mkonge kwa wakulima wadogo nchi nzima ili zao litumike katika kuwaongezea wananchi kipato kutokana na sifa za mkonge kama zifuatazo;
i)                    Zao la mkonge linavumilia sana ukame
ii)                  Ni zao ambalo halina msimu maalumu wa kupanda hivyo kupelekea kuweza kupandwa wakati wowote na pia halina wakati maalumu wa kuvunwa pale linapokuwa tayari kuvunwa
iii)                Zao la mkonge linaweza kuchanganywa na mazao mengine ya msimu kama kunde, mahindi, maharage , alizeti, njegere na karanga.
iv)                Ni zao ambalo halina uhaba wa vipando.
v)                  Bidhaa zitokanazo na mkonge zinaweza kutumika katika tasnia ya kilimo, nishati, ujenzi, famasia, magari, meli, majumbani,ofisini na mazingira
vi)                Mmea wa mkonge unaweza kuishi kwa kipindi cha miaka 10-25 hivyo kumuhakikishia mkulima kipato cha uhakika
vii)                Mkonge  ni zao linalo staimil magonjwa,  wadudu na  maguu na hata upungufu wa rutuba kwenye udongo.

UZALISHAJI WA MKONGE
Kilimo bora cha zao la mkonge ni muhimu ili kuongeza tija kwa mkulima . kumbukumbu tulizonazo ni kwamba wenzetu Uchina wanavuna tani 4-5 kwa hekta kwa kuboresha kilimo hicho ukilinganisha na  tani 1-2 kwa hecta hapa Tanzania. Ivyo ni muhimu tuboreshe kilimo chetu ili tuweze kupata mavuno mengi na kwa hiyo kushindana na wenzetu kwenye soko la kimataifa. Mambo yafuatayo ni yakuzingatia katika uzalishaji wa mkonge;
i)                    Maandalizi ya miche bora ya mkonge
ii)                  Utunzaji wa vitalu vya mkonge
iii)                 Upandaji wa mkonge shambani
iv)                Utunzaji wa mkonge shambani
v)                  Kilimo mseto cha mkonge na mazao mengine yachakula
i)                    MAANDALIZI YA VITALU VYA MKONGE
Uchaguzi sahihi wa miche ya mkonge na maadalizi ya mazuri ya kitalu kwa ajili ya upandaji wa miche ya mkonge ni muhimu kwa ukuaji haraka na hatimaye utoaji wa mavuno bora na mengi ya zao la mkonge.
Kuna aina nne ya vipando vya mkonge;
·         Vikonyo  (bulbils) huota kwenye mlingoti baada ya maua ya mkonge kupukutika
·         Machipukizi (suckers) huchipua kutoka kwenye mmea wa mkonge
·         Miche inayozalishwe ndani ya maabara kwa njia ya tissue culture (mtc lab)
·         Miche inayotokana na mizizi au tumba za mkonge huitwa rhizomes japo aina hii ya miche sasa hivi haitumiki sana hapa nchini.
ii)                  Utunzaji wa vitalu vya mkonge
·         Palizi –upaliliaji kwa jembe la mkono kwa kawaida palizi linaweza kufanyika mara 4-8 kutegemea na udongo.
-          Upaliliaji kwa kutumia dawa za magugu mfano hy-varax hutumika sana kuzuia magugu katika bustani za mkonge huzuia uotaji wa magugu kwa muda wa miezi sita mfululizo ambayo utumika kwa kiasi cha kilo 4.5/ha nah ii dawa inashauriwa inyunyiziwe bustanini wakati udongo una unyevunyevu.
·         Namna ya kurutubisha vitalu
-          Taka za mkonge ( sisal waste)
-          Mbolea ya chunvichunvi zenye kirutubisho cha nitrogen 30kg /ha  kama CAN, SA, and UREA kwa kukuzia
-          Mbolea aina ya potash kama MOP  na DAP
-          Wadudu na magonjwa ya mkonge kama tembo wa mkonge ( sisal weevil)  na scale na magonjwa kama kuoza kwa mashina (bole rot) , ugonjwa wa pundamilia (zebra leaf rot) na ugonjwa wa mabaka kwenye majani (korogwe leaf sport)
iii)                UPANDAJI WA MKONGE SHAMBANI
·         Uchaguzi na upandaji wa miche ya kupanda (grading) ukubwa wa miche ya kupanda ni bora iwe na urefu kati ya sentimita 50-70 na uzito kati ya kilo 2-4 miche ipangwe katika madaraja kufuatana na ukubwa
-          Uchimbaji wa miche huchimbwa kwa kutumia jembe  au sululu ili kitunguu (bole) kisikatwe ili kuepusha kushambuliwa na wadudu.
-          Kutayarisha miche kwa kukata mizizi bila kuaribu shina na majani yaliyonyauka yaondolewe
-          Upandaji wa kutumia machipukizi (suckers) ikusanywe kutoka katika mashamba yenye mkonge mdogo si zaidi ya mikato 2
-          Kuligawa shamba katika maboma kwa ajili ya kupanda mkonge shambani
·         Mifumo ya kupanda mkonge shambani
-          Mstari mmoja (single row) kwa nafasi ya 3.5 x 0.75 mita
-          Upandaji wa mistari miwili (double row ) upandaji huu miraba miwili huwekwa karibu ili kutoa nafasi pana kati ya miraba hiyo. Nafasi ya upandaji utegemea aina ya mkonge
Ø  Mkonge aina ya sisalana nafasi pana ni mita 3.5 na nafasi kati ya mistari miwili iliyo karibu ni mita 1 wakati nafasi kati ya mmea mmoja na mwingine ni setimita 90 (3.5 +1 x 0.9) mita. Hutoa mimea 5,000 kwa hekta.
Ø  Mkonge chotara (H.11648) nafasi pana ni mita 4 na nafasi kati ya mistari iliyo karibu ni 1 pia nafasi  kati ya mmea mmoja na mwingine ni mita 1 (4 +1 x 1) mita. Upandaji huu utoa mimea 4,000 kwa hekta.
·         Muda wa kupanda inashauriwa kupanda mkonge kabla mvua hazijaanza na mkonge upandwe kina cha sentimita 8 ardhini na kushindiliwa
iv)                UTUNZAJI WA MKONGE SHAMBANI
                         Ili mkulima wa mkonge apate mavuno mengi ni vyema kuzingatia yafuatayo
-       Matumizi ya taka za mkonge (sisal waste) ili kuifadhi unyevunyevu na kurutubisha udongo.
-       Matumizi ya chokaa (agriculture lime) ili kuongeza chachu pH mpaka 5.5-5.8 inayotakiwa na mkonge.
-       Kuweka mbolea za chunvichunvi zenye kirutubisha cha nitrogeni mfano CAN UREA, potasiam  na phosphorus kama MOP, TSP NA DAP.
-       Udhibiti wa magugu ili kuepusha kutumia maji na virutubisho vinavyotakiwa kutumiwa na mmea. Kwakutumia njia zifuatazo;- kutumia jembe au nyengo, kutumia madawa mfano bromacil, kutumia jamii ya mikunde (cover crop) mfano tropical kudzu.
v)                   KILIMO   MSETO CHA MKONGE NA MAZAO MENGINE YA CHAKULA
Eneo linalotumiwa kwa mkonge ni asilimia 60 na kiasi kilichosalia asilimia 40 hubaki tupu ivyo ni bora Kulima na mazao mengine faida za Kilimo mseto
-          Kutumia ardhi kwa ufanisi
-          Kuzalisha mazao Zaidi ya moja katika eneo hilo na kwa Gharama ndogo.
-          Kwa kupanda mazao jamii ya kunde husaidia kuongeza rutuba ya udongo.
-          Kupata Chakula hasa kwa wakulima wadogo na kwa mazao yanayofunika ardhi na kupunguza mmomonyoko wa ardhi kwa njia ya upepo na maji.
·         Mazao yanayofaa kuchanganywa na mkonge maharage, kunde, karanga, soya, choroko alizeti, ufuta, mahindi nk
·         Mazao yasiyofaa kuchanganywa na mkonge ni mazao ya kudumu kama migomba, minazi, mikorosho na michungwa mtama  uwele viazi vitamu na mihogo

2. UVUNAJI WA MKONGE
i)        Ukataji wa mkonge ili kupata singe mkonge uvunwa majani kwa kuzingatia yafuatayo
-             Jani linalovunwa ni lazima liwe na urefu unaozidi sentimeta 90
-             Ni lazima jani liwe na mwanguko usiozidi digrii 45%
-             Ni lazima likatwe kwenye shingo yake
-             Ni marufuku kukata kitunguu au mape
ii)      Usombaji wa majani yaliyokatwa
iii)    Usindikaji
iv)    Kulainisha singa (brushing)
v)      Kufunga mizingo kwenye press (pressing machine)
vi)    Kupanga madaraja ya singa (grading) kwa kuangalia urefu wa singa narangi ya singa

IMEANDALIWA NA; MR. MBARAKA BATARE
MUTAFITI WA MKONGE
ARI-MLINGANO TANGA TANZANI

SIMU; 0769323117/0717698998

Maoni 29 :

  1. nimeipenda mimi ntemange bujiku namba yangu ni 0763099028 na barua pepe ni ntemangeb@gmail.com naomba ushauri niko shinyanga

    JibuFuta
  2. Nimeipenda ubarikiwe sana, mimi naitwa Yassin Manota, nipo morogoro nataka nipande katani hekar 20. Namba yangu ya sim ni 0756463833 na mail yangu ni yassnota@gmail.com naomba nisaidie soft copy ya makala hii na nyingi kama zipo kwa sisi tunaoanza.

    JibuFuta
  3. Hongera kwa kutupa darasa,ubarikiwe sana,vipi kuhusu masoko na bei ya mkonge kiongozi!

    JibuFuta
  4. Asante kwa darasa.nauliza mkoani ruvuma wilaya ya mbinga mikonge inastawi?

    JibuFuta
  5. Asante sana kwa kutupa darasa kwa sisi tunaoanza kilimo hiki cha Mkonge.

    JibuFuta
  6. Shukura sana Kwa elimu juu ya zao LA mkonge.

    JibuFuta
  7. NAHITAJI MBEGU BORA ZA MKONGE NAPATAJE? MIMI NIKO SINGIDA VIJIJINI KWA NAMBA 0752795267

    JibuFuta
  8. Naomba maelekezo zaidi namna ya kulima zao hili, nipo Kigoma

    JibuFuta
  9. Uoande wa gharama na faida kwenye uwekezaji wa mkonge ni zipi kwa hekari 1

    JibuFuta
  10. Hekari kumi10 za mkonge Kwa sasa zaweza kutoa tani ngapi pia naweza kuuza Kwa bei gani?. Naombeni mnijuze.

    JibuFuta
  11. Nilitaka kujua zao la mionge linachukua muda gani toka kupanda mpaka kuanza kuvuna especially kwa mbegu ya chotara???

    JibuFuta
    Majibu
    1. Miaka 3 ndio unaanza kuvuna

      Futa
  12. Na mkulima anaweza kupata faida kiasi gani kwa hekari moja ambayo imehudumiwa vizuri??!

    JibuFuta
  13. Nimefatilia vzr kipindi cha tari mkonge
    Nimeupenda , niko tabora nataka mbegu bora za muda mfupi zinauzwa bei gani maana namuona waziri mkuu kassim kahamasisha kweli nami nimependa , nipo tabora mjini ninahekali 2 nata nipande mkonge naomba mbegu nizipate , namba zangu ni
    0689997575
    0769368615

    JibuFuta
  14. Nielimu nizuli san tunakushukur san mtalam

    JibuFuta
  15. Nitumie makala hii kupitia

    rashidntolok@gmail.com

    JibuFuta
  16. Hii ni mada nzuri sana kwa maendeleo ya kilimo na kupunguza umaskini wa mkulima

    JibuFuta
  17. Maelezo yako ya kitaalamu yanahamasisha sana na kututia moyo wa kushiriki katika kulifufua zao la Mkonge, kwa manufaa yetu na Taifa kwa ujumla. Binafisi ninalo eneo kama ekari 20 ningependa nilime zao hilo kwa kutumia mbegu mpya za " Hybrid " je utaratibu wenu wa kuzipata ukoje? Mob: 0782 780389 ( Msuwakollo)

    JibuFuta
  18. Maelezo yako ya kitaalamu yanahamasisha sana na kututia moyo wa kushiriki katika kulifufua zao la Mkonge, kwa manufaa yetu na Taifa kwa ujumla. Binafisi ninalo eneo kama ekari 20 ningependa nilime zao hilo kwa kutumia mbegu mpya za " Hybrid " je utaratibu wenu wa kuzipata ukoje? Mob: 0782 780389 ( Msuwakollo)

    JibuFuta
  19. Maelezo yako ya kitaalamu yanahamasisha sana na kututia moyo wa kushiriki katika kulifufua zao la Mkonge, kwa manufaa yetu na Taifa kwa ujumla. Binafisi ninalo eneo kama ekari 20 ningependa nilime zao hilo kwa kutumia mbegu mpya za " Hybrid " je utaratibu wenu wa kuzipata ukoje? Mob: 0782 780389 ( Msuwakollo)

    JibuFuta
  20. Mimi Ntemange Bujiku ninaipenda biashara ya mkonge lakini nashindwa kuzipata mbegu za mkonge naomba nisaidiwe Niko kishapu shy

    JibuFuta
  21. Ebu nieleweshe vizuri kwenye nafasi za kupandia

    JibuFuta
  22. Casino - Mapyro
    Casino Hotel Map and reviews. Casino 논산 출장마사지 Resort, 경산 출장안마 Laughlin. Phone Number, 1-800-522-4700. Hours, Mon-Fri 9:00 am - 계룡 출장마사지 9:00 pm. Directions, 김제 출장안마 1-888-522-4700. Casino Address, 777 Casino Parkway. Map 남원 출장샵

    JibuFuta